Maandiko ya Kiebrania (MRS 001)
(MRS001sw)

Course Summary

Karibu kwa kosi hii ya masomo katika maandiko ya kiebrania. Ndiyo kosi ya kwanza katika tuzo zifuatazo za masomo yaliyo katika chuo cha NationsUniversity: Cheti cha masomo ya Dini, cheti (duni kuliko Diploma) cha masomo ya Dini, Diploma ya masomo ya Dini, shahada ya kwanza katika masomo ya dini na shahada ya pili katika masomo ya dini. Mwanafunzi akifaulu kukamilisha kosi hii, atatuzwa masaa matano (5) kwa muhula wa kukamilisha kosi kabla ya kuhitimu shahada au alama tatu (3) za kuonyesha kuwa amekamilisha kosi baada ya kuhitimu shahada ya kwanza.

Mpango wa Kosi

BRS 1 Maandiko ya kiebrania inatutanguliza yaliyomo katika Agano la Kale. Kosi ina sehemu tano: (1) Sheria, (2) Manabii wa awali, (3) Manabii waliokuja baadaye, (4) Maandishi: Historian na (5) Maandishi: Hekima na Ibada. Kila mtihani utakamilishwa kwa kunyakua alama zinazohitajika baada ya kufanya mtihani huo hwa kusimamiwa.

Ustadi

Kiwango cha BRS 1 Maandiko ya Kiebrania kitafikiwa iwapo mwanafunzi ataweza kufanya yafuatayo:

1. Uwezo wa kutambua angalau wahusika 110 katika Agano la Kale.

2. Uwezo wa kutambua maeneo muhimu ya kijiografia.

3. Uwezo wa kuonyesha ufahamu wa kijumla kuhusu hadithi, matukio, yaliyomo na ujumbe wa kiunabii ulio katika kila kitabu cha Agano la kale.

4. Uwezo wa kuratibu wahusika wakuu na matukio makuu kulingana na jinsi walifuatana/yalifuatana kutoka kipindi kimoja hadi kingine.

Vifaa

Kitabu ambacho mwanafunzi atahitaji kwa ajili ya kosi hii ni Biblia tu. Biblia Takatifu (union version) ndiyo inapendekezwa sana kwa kusoma. Maswali ya mtihani yatachukua mtindo wa lugha na mwendelezo wa maneno wa tafsiri hii. Hata hivyo, ikiwa mwanafunzi ana tafsiri nyingine yoyote ya Kiswahili, itakuwa sawa.

Mifano ya Maswali ya Mtihani

1. Mwanadamu wa kwanza alikuwa: (A) Haruni, (B) Ibrahim, (C) Adamu, (D) Musa, (E) Zakaria.

2. Mto uliotoka katika bustani ya Edeni na ukagawanyika kuelekea kwa Mto huu: (A) Haruni, (B) Yordani, (C) Nile, (D) Mto wa Misri, (E) Hidekeli.

Maswali yote ya mtihani ni ya kuchagua jibu moja tu

Kukadiri Mtihani

Wakati mitihani yote mitano imekamilika, gredi ya kosi nzima itapewa. Gredi hiyo inaweza kuwa "A," "B," au "C." Kwa yoyote ile, ni vyema kuonyesha iwapo matokeo ni bora zaidi, bora au wastani. Gredi hiyo itatokana na alama za mitihani yote mitano, zitakazowekwa pamoja, kisha kugawanywa na tano. Hata hivyo, alama chini ya asilimia sabini (70%) hazitakubaliwa, katika mtihani wowote ule. Kuna ruhusa ya kurudia mtihani, lakini si zaidi ya majaribio mengine mawili. Katika hali ambapo mwanafunzi hakamilishi kosi mwaka mmoja baada ya tarehe ya kujisajilisha, ataandikiwa alama ya "I" (kutokamilisha), katika karatasi rasmi ya matokeo yake ya mtihani. Iwapo mwanafunzi amepata "I" na angependa kujisajilisha upya kwa kosi hiyo, atafuata sheria zozote mpya ambazo zimekuwa zikifuatwa tangu wakati alijisajilisha awali.