Maandiko ya Kiyunani (MRS 006)
(MRS006sw)
Course Summary
Karibu kwenye kosi hii ya masomo katika maandiko ya Kiyunani. Hii ni kosi ya pili katika ratiba ya Shahada ya Dini (B.R.S.). Mwanafunzi akimaliza kosi hii kwa kuhitimu vizuri, atatuzwa saa 5 kwa muhula kwa wale ambao hawajahitimu au.
Mpangilio wa kosi
BRS 2 Maandiko ya Kiyunani ni utangulizi wa ukweli uliyomo katika Agano Jipya. Kosi imepangiwa katika masomo matano: (1) Injili, (2) Matendo ya Mitume, (3) Barua za Paulo, (4) Nyaraka za kawaida na ufunuo, na (5) Nyaraka—Kiini cha yaliyomo. Kila funzo litakamilika kwa kupata alama maalum kwenye mtihani uliosimamiwa.
Ustadi
Kigezo kwa BRS 2 Maandiko ya Kiyunani ni kupata stadi zifuatazo:
1. Uwezo wa kufahamu wahusika 75 wanaotambulika katika Agano Jipya.
2. Uwezo wa kutambua mandhari kuu za kijiografia
3. Kufahamu yaliyomo katika kila kitabu cha Agano Jipya
4. Kufahamu kwa jumla ujumbe uliyomo katika Agano Jipya
Vifaa
Kitabu cha pekee ambacho mwanafunzi atahitaji katika kosi hii ni Biblia. Tafsiri ya Biblia Takatifu imependekezwa sana katika masomo haya. Maswali ya mtihani yatatumia lugha na maendelezo kutoka kwa tafsiri hiyo. Hata hivyo, hatutakuwa na matatizo ukitumia Biblia nyingine tofauti.
Mfano wa Maswali ya Mtihani
1. Mafundisho ya Yesu yalilenga
(A) Nafsi, (B) Watu wote, (C) Mafarisayo, (D) Masadukayo, (E) Waandishi
2. Nyaraka nyingi ziliandikwa na mtu huyu kuliko mtu mwingine yeyote
(A) Yakobo (B) Yohana . (C) Paulo, (D), Petro, (E) Timotheo
Maswali yote ya mtihani ni ya kuchagua.
Uwekaji Viwango
Mitihani yote mitano ikimalizika, daraja ya kosi itatolewa. Daraja yaweza kuwa “A,” “B,” au “C,” kutegemea ikiwa kosi ilikuwa mufti, nzuri au wastani. Daraja itategemea kimo cha katikati cha masomo yote matano. Hata hivyo hakuna chini ya 70% itakayokubaliwa kwa mtihani wowote. Mtihani unakubaliwa kurudiwa mara mbili tu. Iwapo mwanafunzi hatakamilisha kosi katika mwaka mmoja kuanzia tarehe ya kujiandikisha, herufi “I” (kutokamilisha) itawekwa kwa nakala rasmi. Iwapo mwanafunzi amepata “I” na angependa kujiandikisha tena kwa kosi, atahitajika tena kufuata sheria mpya ambazo zilitumika alipojiandikisha mwanzoni.